Mfuko wa Wekeza Maisha

Mfuko wa Wekeza Maisha ni mfuko wa pili kuanzishwa na UTT AMIS na ulizinduliwa mnamo tarehe 16 Mei 2007. Mfuko ulitimiza miaka 10 na kuiva mwaka 2017. Mfuko wa Wekeza Maisha unatoa faida za aina 2 ambazo ni, faida ya kukuza mtaji, pamoja na bima ya maisha kwa wawekezaji. Mfuko unawekeza katika hisa zilizoorodheshwa na maeneo yenye vipato vya kudumu.

MALENGO YA MFUKO

Ni mfuko wa wazi wenye lengo la kukuza mtaji  na kutoa faida za; bima ya maisha, bima ya ajali, bima ya ulemavu wa kudumu na gharama za mazishi. Zaidi ya 99% za fedha za wawekezaji wa mfuko wa Wekeza Maisha huwekezwa kwenye masoko mbalimbali ya fedha na 1% ni kwa ajili ya malipo ya bima.

NANI ANARUHUSIWA KUWEKEZA NA UMRI WA KUINGIA.

Mfuko uko wazi kwa mtanzania mkazi na asiye mkazi mwenye umri wa miaka 18 hadi 55.

UKWASI/KUUZA VIPANDE

Mwekezaji ataruhusiwa kutoa sehemu ya uwekezaji wake baada ya kudumu kwa miaka 5 katika uwekezaji na ataruhusiwa kutoa kiasi chote baada ya kudumu kwa miaka kumi katika uwekezaji.

Malipo ya mauzo ya vipande yatashughulikiwa ndani ya 10 za kazi baada ya kupokelewa. Fedha zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji.

SERA YA MFUKO

Mfuko unaruhusiwa kuwekeza kwenye hisa zilizoorodheshwa, ikizingatiwa kuwa kiasi cha pesa kitakachowekezwa kwenye sehemu hiyo kisizidi 40% ya uwekezaji wote wa mfuko na 60% iliyobaki huwekezwa kwenye dhamana mbalimbali za serikali zenye ukomo tofauti, hatifungani za kampuni binafsi, na kwenye akaunti za amana.

SIFA ZA MFUKO

  • Watu binafsi wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga.
  • Mfuko unaruhusu umiliki wa mtu binafsi tu.
  • Mfuko unatoa fursa za aina mbili za mpango wa kuchangia/kuwekeza:

(a) Kuchangia kwa awamu na

(b) Kuchangia kwa mkupuo

  • Vipande vinauzwa kwa thamani halisi ya wakati huo [hakuna gharama za kujiunga].
  • Mfuko unampa fursa mwekezaji kuwekeza kwa mpangilio maalum. Mwekezaji anaweza kuchagua kuchangia kila mwezi, mara mbili kwa mwaka au mara moja kwa mwaka.
  • Kiwango cha kuwekeza:
  1. Kiwango cha chini kwa uwekezaji kwa miaka kumi ni TZS. 1,000,000 ambacho kinaweza kuwekezwa kwa awamu au kwa mkupuo.
  2. Kiwango cha chini cha uwekezaji wa awamu ni TZS.8,340 kila mwezi.

(c) Hakuna kiwango cha juu cha uwekezaji, lakini mafao ya bima ya maisha hayatazidi TZS. 25,000,000.

  • Gharama za kujitoa kwenye mfuko;

a) 2% ya bei ya kipande baada ya miaka 5.

b) Hakuna gharama za kutoka baada ya miaka 10.

  • Mafao ya bima yanayopatikana ni: - Bima ya maisha, bima ya ulemavu wa kudumu na bima ya ajali.

Mafao ya bima ya maisha – Kifo au ulemavu wa kudumu.

  1. Mpango wa kuwekeza kwa awamu: Kinga ya Bima ya maisha ina thamani sawa na kiasi kisicholipwa na mwekezaji kwa muda uliosalia katika mpango wake wa uwekezaji. (Muhimu: Kiwango cha juu kitakacholipwa ni TZS. 25,000,000).
  2. Mpango wa kuwekeza kwa mkupuo: Kinga ya Bima ya Maisha ina thamani sawa na kiwango alichochagua mwekezaji. (Muhimu: Kiwango cha juu kitakacholipwa ni TZS. 25,000,000).

Mafao ya bima ya ajali: Mwekezaji atalipwa 20% ya kiwango kilichokusudiwa katika mpango wa uwekezaji, hata hivyo kiwango cha juu kitakacholipwa ni TZS. 5,000,000.

Mafao ya Gharama za Mazishi: Kila mwekezaji atalipwa TZS.500,000 kwa ajili ya mazishi endapo atafariki bila kujali kiwango alichowekeza. Mafao haya yatalipwa kwa ajili ya wawekezaji watakaoingia wakati wa mauzo ya mwanzo tu.

  • Kama mwekezaji atakaa kipindi chote cha uwekezaji wake, atapata faida ya mkono wa pongezi ikiwa amechangia michango yote kwa wakati na mwekezaji hakuuza vipande vyake katika kipindi chote cha uwekezaji.

Faida ya mkono wa pongezi ni:

(a) Kwa mpango wa kuchangia kwa awamu - 5% ya kiwango kilichokusudiwa katika mpango wa uwekezaji.

(b) Kwa mpango wa kuchangia kwa mkupuo - 7% ya kiwango kilichokusudiwa katika mpango wa uwekezaji.

  • Vipande katika mfuko huu haviruhusiwi kuhamishwa kutoka kwa mwekezaji mmoja kwenda kwa mwingine, au kutumika kama dhamane ya mkopo.

KIGEZO CHA UFANISI

  • Mjumuiko wa utendaji wa faharisi kwenye soko la hisa la Dar es Salaam pamoja na faida ya dhamana ya serikali ya miaka 7.

JINSI YA KUWEKEZA/KUNUNUA VIPANDE

Kupitia simu yako ya mkononi piga *150*82# kufungua akaunti na kisha kamilisha usajili kwa kujaza fomu na kuifikisha katika ofisi za UTT AMIS au kutuma kwa barua pepe uwekezaji@uttamis.co.tz. Endelea kuwekeza kupitia benki au mitandao ya simu kama M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA na T-PESA.

HALI YA UTENDAJI KWA MFUKO WA WEKEZA MAISHA

Chati Na. 01 Ukubwa wa mfuko wa Wekeza Maisha na thamani ya kipande hadi tarehe 30 Juni 2025

 

Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Wekeza Maisha na Kigezo cha Faida kwa Asilimia/Muda

Faida kwa Asilimia/Muda2022/232023/242024/25
Faida kwa mwaka  hadi kufika Juni12.6%14.8%15.3%
Kigezo linganifu7.6%11.2% 

 

 

 

 

 

Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Wekeza Maisha na Kigezo cha ufanisi kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2022

 

UTT AMIS Connect
Loading...