MFUKO WA JIKIMU

Mfuko wa Jikimu ni mfuko wa nne kuanzishwa na taasisi ya UTT AMIS mnamo tarehe 3 Novemba 2008. Mfuko huu ni mfuko wa wazi ulioanzishwa ili kuwawezesha wawekezaji kupata gawio kila robo mwaka au mara moja kwa mwaka na kutoa fursa ya kukuza mtaji.

MALENGO YA MFUKO

Mfuko huu ni mpango ulio wazi wenye lengo la kukuza na kutoa gawio kutokana na mapato ya ziada katika vipindi tofauti na pia kukuza mtaji kwa mwekezaji wa muda mrefu.

UKWASI/KUUZA VIPANDE.

Malipo ya mauzo ya vipande yatashughulikiwa ndani ya siku 10 za kazi baada ya kupokelewa. Fedha zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji.

WANAORUHUSIWA KUWEKEZA

Wawekezaji wote ikiwa ni pamoja na watu binafsi, taasisi, makampuni, na vikundi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

SERA YA MFUKO

Mfuko unaruhusiwa kuwekeza kwenye hisa zilizoorodheshwa, ikizingatiwa kuwa kiasi cha pesa kitakachowekezwa kwenye sehemu hiyo kisizidi 35% ya uwekezaji wote wa mfuko na 65% iliyobaki itawekezwa kwenye dhamana mbalimbali za serikali zenye ukomo tofauti, hatifungani za kampuni binafsi, na kwenye akaunti za amana.

SIFA ZA MFUKO:

  • Mfuko una mipango mitatu ya uwekezaji kama ifuatavyo:

(a) Mpango wa gawio la robo mwaka [Kiwango cha chini cha uwekezaji ni TZS. 2,000,000]

(b) Mpango wa gawio la mwaka [Kiwango cha chini cha uwekezaji ni TZS. 1,000,000]

(c) Mpango wa mwaka wa kukuza mtaji [Kiwango cha chini cha uwekezaji ni TZS. 5,000]

  • Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza ni:

(a) TZS 15,000 kwenye mpango wa gawio la mwaka au la robo mwaka.

(b) TZS 5,000 kwenye mpango wa kukuza mtaji.

  • Vipande vinauzwa kwa thamani halisi ya wakati huo (hakuna gharama za kujiunga).
  • Umiliki wa mtu mmoja au umiliki wa pamoja unaruhusiwa katika mfuko huu.
  • Ni rahisi kwa mwekezaji kupata fedha pindi atakapozihitaji, (ndani ya siku 10 za kazi baada ya kupokelewa kwa maombi katika ofisi za UTT AMIS).
  • Mwekezaji anaruhusiwa kutoa sehemu ya uwekezaji wake au kiasi chote. Gharama za kujitoa ni kama ifuatavyo:
  • (a) 2% kwa uwekezaji uliodumu kwa kipindi kisichozidi mwaka 1.
  • (b) 1.5% kwa uwekezaji uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya mwaka 1 na chini ya miaka 2.
  • (c) 1.0% kwa uwekezaji uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2 na chini ya miaka 3.
  • (d) Hakuna gharama za kutoka kwa uwekezaji uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 3.
  • Mfuko unaruhusu uhamishaji wa vipande kutoka mwekezaji mmoja kwenda kwa mwekezaji mwingine.
  • Mwekezaji akifariki, mrithi, mwakilishi au mwombaji wa pili ataruhusiwa kuendeleza uwekezaji huo.
  • Vipande vinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo katika tasisi za fedha.

JINSI YA KUWEKEZA/KUNUNUA VIPANDE

Kupitia simu yako ya mkononi piga *150*82# kufungua akaunti na kisha kamilisha usajili kwa kujaza fomu na kuifikisha katika ofisi za UTT AMIS au kutuma kwa barua pepe uwekezaji@uttamis.co.tz. Endelea kuwekeza kupitia benki au mitandao ya simu kama M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA na T-PESA.

KIGEZO CHA UFANISI

  • Mjumuiko wa utendaji wa faharisi kwenye soko la hisa la Dar es Salaam pamoja na faida ya dhamana ya serikali ya miaka 7.

HALI YA UTENDAJI KWA MFUKO WA JIKIMU

Chati Na. 01 Ukubwa wa mfuko wa Jikimu na thamani ya kipande hadi tarehe 30 Juni 2025.

 

Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Jikimu na Kigezo cha ufanisi kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2025.

Mwaka wa Fedha2022/232023/242024/25
Faida kwa mwaka  hadi kufika Juni (baada ya kodi)13.6%13.7%15.5%
Kigezo cha ufanisi7.6%11.2% 
UTT AMIS Connect
Loading...