MFUKO WA HATIFUNGANI

Mfuko wa Hatifungani ni mfuko wa wazi unaowekeza kwenye dhamana za serikali za muda mrefu, hatifungani za kampuni binafsi na kwenye soko la fedha. Mfuko ulianzishwa tarehe 16 Septemba 2019 na hutoa fursa kwa wawekezaji kukuza mtaji pamoja na kupata gawio.

MALENGO YA MFUKO

Mfuko wa hatifungani ni mfuko wa wazi unaolenga kutoa gawio kila mwezi au kila baada ya miezi sita na kumpa mwekezaji fursa ya kukuza mtaji.

UKWASI/KUUZA VIPANDE

Malipo ya mauzo ya vipande yatashughulikiwa ndani ya siku 10 za kazi baada ya kupokelewa. Fedha zitatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mwekezaji.

NANI ANARUHUSIWA KUWEKEZA

Mfuko huu uko wazi kwa mwekezaji mtanzania na asiye mtanzania, aliye ndani au nje ya nchi, watu binafsi (ikijumuisha watoto) na wawekezaji wasio watu binafsi, vikundi na taasisi.

SERA YA MFUKO

Mfuko unaruhusiwa kuwekeza kwenye sehemu zenye vipato vya kudumu. Dhamana zenye mapato ya kudumu zinajumuisha zaidi ya 90% ya uwekezaji na 10% zilizobaki huwekezwa kwenye uwekezaji wenye ukwasi mkubwa.

SIFA ZA MFUKO

  • Mfuko unatoa machaguo matatu ya uwekezaji kama ifuatavyo;
  1. Mpango wa kukuza mtaji
  2. Mpango wa gawio kila mwezi
  3. Mpango wa gawio kila baada ya miezi sita

Kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza:

(a) TZS. 50,000 kwa mpango wa kukuza mtaji;

(b) TZS. 10,000,000 kwa mpango wa gawio kila mwezi; na

(c) TZS. 5,000,000 kwa mpango wa gawio kila baada ya miezi sita.

Kiwango cha chini cha nyongeza katika uwekezaji ni TZS. 5,000 kwa mipango yote ya uwekezaji.

  • Mfuko unawafaa wawekezaji binafsi, taasisi, vikundi au mashirika.
  • Umiliki wa mtu mmoja au umiliki wa pamoja unaruhusiwa katika mfuko huu.
  • Hakuna gharama za kujiunga (entry load) wala kutoka kwenye mfuko (exit load).
  • Mfuko unaruhusu uhamishaji wa vipande kutoka mwekezaji mmoja kwenda kwa mwekezaji mwingine.
  • Mwekezaji akifariki, mrithi, mwakilishi au mwombaji wa pili ataruhusiwa kuendeleza uwekezaji huo.
  • Vipande vinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo katika taasisi za fedha.
  • Hakuna ukomo wa kiwango cha juu cha uwekezaji.

JINSI YA KUWEKEZA/KUNUNUA VIPANDE

Kupitia simu yako ya mkononi piga *150*82# kufungua akaunti na kisha kamilisha usajili kwa kujaza fomu na kuifikisha katika ofisi za UTT AMIS au kuituma kwa barua pepe uwekezaji@uttamis.co.tz. Endelea kuwekeza kupitia benki au mitandao ya simu kama M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA na T-PESA.

KIGEZO CHA UFANISI

  • Wastani wa faida ipatikanayo kwenye Hatifungani ya serikali ya miaka 7 (7 years WAY Treasury bond).

HALI YA UTENDAJI KWA MFUKO WA HATI FUNGANI

 Chati namba 01, Ukuaji wa Mfuko wa Hatifungani tangu kuanzishwa hadi Juni, 2025

 

Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Hatifungani na Kigezo cha ufanisi kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2022.

Mwaka wa Fedha2022/232023/242024/25*
Faida kwa mwaka hadi kufika Juni12.3%12.5%13.4%
Faida ya kigezo cha ufanisi (linganifu)9.7%12.3% 
UTT AMIS Connect
Loading...