MFUKO WA UMOJA.

Mfuko wa Umoja ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na UTT AMIS mnamo tarehe 16 Mei 2005. Umoja ni mfuko wa wazi ambao tangu kuanzishwa kwake mwezi Mei 2005 una zaidi ya miaka 17 sokoni. Mfuko unawekeza katika hisa zilizoorodheshwa na maeneo yenye vipato vya kudumu.

MALENGO YA MFUKO

Mfuko wa Umoja unalenga zaidi wawekezaji wenye malengo ya muda wa kati na mrefu, jambo ambalo huwawezesha kupata muda wa kutosha kujiwekea akiba na kukuza mtaji kupitia uwekezaji.

Mfuko wa Umoja humpa mwekezaji hamasa na kumjengea desturi ya kujiwekea akiba na kupata faida itokanayo na uwekezaji kwenye soko la mitaji na dhamana nchini.

UKWASI/KUUZA VIPANDE

Malipo ya mauzo ya vipande yatashughulikiwa ndani ya 10 za kazi baada ya kupokelewa. Fedha zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji.

NANI ANARUHUSIWA KUWEKEZA

Wawekezaji wote ikiwa ni pamoja na watu binafsi, taasisi, makampuni, na vikundi vya jumuiya ya Afrika mashariki (EAC).

SERA YA MFUKO

Mfuko unaruhusiwa kuwekeza kwenye hisa zilizoorodheshwa, ikizingatiwa kuwa kiasi cha pesa kitakachowekezwa kwenye sehemu hiyo kisizidi 50% ya uwekezaji wote wa mfuko na 50% inayobaki itawekezwa kwenye dhamana mbalimbali za serikali zenye ukomo tofauti, hatifungani za kampuni binafsi, na kwenye akaunti za amana.

 

SIFA ZA MFUKO WA UMOJA

  • Vipande vinauzwa kwa thamani halisi [hakuna gharama za kujiunga].
  • Umiliki wa mtu mmoja au umiliki wa pamoja unaruhusiwa katika mfuko huu.
  • Kiwango cha chini cha kujiunga ni vipande 10 tu.
  • Gharama ya kujiondoa inayotozwa ni 1% ya thamani halisi ya kipande.
  • Urahisi wa kujiunga na kutoka – manunuzi na mauzo hufanyika kila siku ya kazi.
  • Mauzo ya vipande yanaruhusiwa na mwekezaji atapata fedha ndani ya siku 10 za kazi baada ya ombi la kuuza vipande kupokelewa katika ofisi za UTT-AMIS.
  • Mfuko unaruhusu uhamishaji wa vipande kutoka mwekezaji mmoja kwenda kwa mwekezaji mwingine.
  • Mwekezaji akifariki, mrithi, mwakilishi, au mwombaji wa pili ataruhusiwa kuendeleza uwekezaji huo.
  • Vipande vinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo katika taasisi za fedha.
  • Hakuna kiwango cha juu cha uwekezaji.

 

JINSI YA KUWEKEZA/KUNUNUA VIPANDE

Kupitia simu yako ya mkononi piga *150*82# kufungua akaunti na kisha kamilisha usajili kwa kujaza fomu na kuifikisha katika ofisi za UTT AMIS au kutuma kwa barua pepe uwekezaji@uttamis.co.tz. Endelea kuwekeza kupitia benki au mitandao ya simu kama M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA na T-PESA.

KIGEZO CHA UFANISI

  • Mjumuiko wa utendaji wa Faharisi kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam pamoja na faida ya dhamana ya serikali ya miaka 7.

HALI YA UTENDAJI KWA MFUKO WA UMOJA

Chati Na. 01 Ukubwa wa mfuko wa Umoja na thamani ya kipande hadi tarehe 30 Juni 2025

 

Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Umoja na Kigezo cha ufanisi kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni

Mwaka wa Fedha2022/232023/242024/25
Faida kwa mwaka hadi kufika Juni11.2%12.1%13.3%
Faida ya kigezo cha ufanisi (linganifu)7.6%11.25% 

 

 

 

 

UTT AMIS Connect
Loading...