
Profesa Faustine Kamuzora (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala (kulia), katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali.
Katika mwaka wa fedha 2025/26, UTT AMIS imeikabidhi Serikali gawio la shilingi bilioni 11, ikiwa ni ongezeko kutoka shilingi bilioni 7 zilizotolewa mwaka wa fedha 2024/25. Hatua hii inaakisi ukuaji endelevu wa taasisi na mchango wake katika kuongeza mapato ya Serikali kupitia uwekezaji wenye tija na usimamizi madhubuti wa rasilimali za wawekezaji.

