
Mfuko wa Watoto ni mfuko wa tatu kuanzishwa na UTT AMIS mnamo tarehe 1 Octoba, 2008. UTT AMIS inatambua umuhimu wa mtoto katika maendeleo ya taifa siku zijazo. Kwa sababu hiyo, mfuko wa watoto (Watoto Fund) ulizinduliwa. Mfuko wa watoto ni suluhisho la kifedha kupitia uwekezaji ambalo linalenga katika kukuza mtaji kwa faida ya muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya watoto wetu wapendwa.
MALENGO YA MFUKO
Mfuko wa watoto ni mfuko wa wazi unaowafaa wawekezaji wenye lengo la kukuza mtaji kupitia kuwekeza pesa kwenye hisa zilizoorodheshwa na maeneo yenye mapato ya kudumu. Kila mzazi/Mlezi angependa mwanae;
- Awe na furaha ya kudumu;
- Awe na hisia nzuri katika maisha yake;
- Apate kazi bora na nzuri;
- Aweze kujitegemea kutokana na kipato chake.
Jibu la maswali hayo ni moja tu; wekeza katika mfuko wa watoto
Mfuko una aina mbili za uwekezaji:
- Kulipia ada za masomo- Mpango huu ni kwa ajili ya malipo ya ada ya masomo ya mtoto.
- Kukuza mtaji – Mpango huu ni wa kukuza mtaji wa mtoto ambae ndiye mwekezaji.
NANI ANARUHUSIWA KUWEKEZA:
- Mzazi/Mlezi kwa jina la mtoto ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18.
- Taasisi, kampuni na vikundi vinaweza kuwawekezea watoto kama sehemu ya huduma kwa jamii.
UKWASI/KUUZA VIPANDE
Mwekezaji anaweza kuuza vipande vyote au baadhi ya vipande baada ya mtoto kutimiza umri wa miaka 12. Malipo ya mauzo ya vipande yatashughulikiwa ndani ya 10 za kazi baada ya kupokelewa.
SIFA ZA MFUKO
- Uwekezaji unafanywa kwa jina la mtoto aliye chini ya miaka 18.
- Mfuko unaruhusu umiliki wa mtu binafsi tu.
- Kiwango cha chini cha uwekezaji ni TZS. 10,000.
- Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza ni TZS. 5,000.
- Hakuna kiwango cha juu cha uwekezaji.
- Vipande vinauzwa kwa thamani halisi ya wakati huo [hakuna gharama za kujiunga].
- Gharama za kutoka;
(a) 1% ya thamani ya kipande kwa uwekezaji uliodumu kwa kipindi kisichozidi miaka 3.
(b) Hakuna gharama za kutoka endapo uwekezaji utadumu zaidi ya miaka 3.
- Mfuko una mipango miwili ya uwekezaji kama ifuatavyo:
- Mpango wa malipo ya ada ya masomo (scholarship option) –
Malipo ya ada yatalipwa kwa awamu mbili, kila nusu mwaka au kila mwaka kwa ajili ya mtoto, baada ya kufikisha umri wa miaka 12. Madhumuni ya kupokea malipo haya ni kukidhi gharama za ada ya shule ya sekondari au elimu ya juu.
b) Mpango wa kukuza mtaji (growth option) - Mwekezaji hatapata malipo ya mara kwa mara na badala yake mwekezaji atafaidika na ukuaji wa mtaji unaotokana na kukua kwa thamani halisi ya kipande.
- Mwekezaji anaruhusiwa kuuzaa vipande vyake pindi mtoto anapofikisha umri wa miaka 12.
- Mfuko unaruhusu uhamishaji wa vipande kutoka mwekezaji mmoja kwenda mwekezaji mwingine.
- Mwekezaji akifariki, mrithi ataruhusiwa kuendeleza uwekezaji huo.
- Vipande vinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo katika taasisi za fedha.
- Kupevuka kwa mpango wa mwekezaji (Ukomo).
Ingawa mfuko ni endelevu (hauna ukomo), uwekezaji kwa mtoto mnufaika utafikia ukomo pindi atakapotimiza umri wa miaka 24. Uwekezaji huo unapopevuka kila mwenye vipande ana uhuru wa kuchagua kati ya mambo yafuatayo:
a) Kudai thamani ya vipande vyake kwenye mfuko kwa thamani ya wakati huo.
b) Kuwekeza tena kwa kupitia mtoto mbadala (mwenye umri chini ya miaka 18),
c) Kuhamishia vipande vyake kwenye mfuko mwingine wowote unaoendeshwa na UTT AMIS.
JINSI YA KUWEKEZA/KUNUNUA VIPANDE
Kupitia simu yako ya mkononi piga *150*82# kufungua akaunti na kisha kamilisha usajili kwa kujaza fomu na kuifikisha katika ofisi za UTT AMIS au kutuma kwa barua pepe uwekezaji@uttamis.co.tz. Endelea kuwekeza kupitia benki au mitandao ya simu kama M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA na T-PESA.
KIGEZO CHA UFANISI
Mjumuiko wa utendaji wa faharisi kwenye soko la hisa la Dar es Salaam pamoja na faida ya dhamana ya serikali ya miaka 7.
HALI YA UTENDAJI KWA MFUKO WA JIKIMU
Chati Na. 01 Ukubwa wa mfuko wa Jikimu na thamani ya kipande hadi tarehe 30 Juni 2025
Jedwari Na. 01 Viwango vya Faida kwa mfuko wa Jikimu na Kigezo cha ufanisi kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2025
| Mwaka wa Fedha (Baada ya kodi) | 2022/23 | 2023/24 | 2024/25 |
| Faida kwa Asilimia/Muda | 12.4% | 14.1% | 15.8% |
| Faida kwa mwaka hadi kufika Juni | 7.6% | 11.2% |

