Mkurugenzi wa Uwekezaji

Bibi Pamela ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara kutoka ESAMI na pia anashahada ya kwanza ya biashara kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Bibi Pamela pia amehudhuria kozi mbalimbali ikiwemo mshauri katika mambo ya uwekezaji kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na amethibitishwa katika kufanya kazi mbalimbali katika soko la hisa la Dar es salaam pamoja na soko la bidhaa (commodity Exchange). Bibi Pamela anashughulika na shughuli zote za uwekezaji ikiwemo kuchambua maendeleo ya soko na kufanya uwekezaji katika Hisa, Dhamana za Serikali pamoja na makampuni yaliyoorodheshwa katika soko la Hisa la Dar es salaam. Pia hufuatilia soko la fedha ili kuona fursa stahiki ambako uwekezaji unaweza kufanyika ili kukuza kipato huku akizingatia hatari zote katika uwekezaji huo. Kabla ya kujiunga na UTT AMIS, Bibi Pamela alifanya kazi na Commecial Bank of Afrika

pamoja na Rasilimali Limited ambao ni mawakala wakubwa wa soko la Hisa Dar es salaam.