Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara

Bwana Wahichinenda ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara, ana shahada ya kwanza ya Sanaa katika takwimu na pia ana shahada ya uzamili ya sayansi katika masuala ya fedha aliyoipata kutoka katika chuo kikuu cha Strathclyde, Glasgow, Scotland. Bwana Wahichinenda kama Mkurugenzi wa uendeshaji anashughulikia masuala yote yanayohusu huduma kwa wawekezaji kwa kipindi kisichopungua miaka saba. Ni mtaalamu mbobezi katika biashara ya huduma za kifedha ambapo uzoefu huo aliupata katika nafasi mbalimbali alizohudumu katika benki ikiwamo Afrikan Banking Corporation Tanzania Ltd alikofanya kazi kama Meneja mikopo.